BADO NAIPENDA YANGA
Written by Living Tarimo on June 8, 2023

Mchezaji mpya wa klabu ya soka ya Azam FC Feisal Salum ‘Fei Toto’ ameushukuru uongozi wa klabu ya Yanga na mashabiki wake kwa kipindi chote walichokuwa pamoja akiwa katika klabu hiyo.
Feisal ametoa shukrani hizo baada ya kusaini mkataba wa kuitumikia Azam FC na kusema “Napenda sana kuwashukuru viongozi wa Yanga pamoja na mashabiki wake kwa kipindi chote nilichokuwa, kwa hiyo mimi nawatakia kila la heri, mimi bado naipenda Yanga na nawapenda asanteni sana”.