BUNGE LAJADILI UNUNUZI WA MAHINDI
Written by Living Tarimo on June 23, 2023

Bunge limeahirisha ratiba ya shughuli zake za siku kwa muda mfupi ili kutoa nafasi ya kujadiliwa suala la ununuzi wa mahindi na utaratibu wa kusafirisha mazao hayo kwenda nje ya nchi.
Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson ametoa nafasi hiyo baada ya wabunge kuibua hoja kuwa licha ya kwamba Serikali ilitoa maagizo kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kuanza kununua mazao, baadhi ya maeneo zoezi hilo halijaanza.
Hata hivyo, Serikali Juni 22, 2023 ilisisitiza kwa mara nyingine kuwa haijazuia usafirishaji wa mazao nje ya nchi, lakini badala yake imezuia usafirishaji mazao nje ya nchi kinyume na utaratibu.