DKT TULIA AMPA MAUA YAKE BONGO ZOZO

Written by on June 19, 2023

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amempongeza Balozi wa Utalii Tanzania, Nicky Reynolds, maarufu kwa jina Bongo Zozo kwa namna ambavyo amekuwa akiitangaza Tanzania pamoja na hamasa yake kwa timu za Taifa hasa zinapokwenda kwenye michezo nje ya nchi.
Dkt. Tulia ametoa pongezi hizo bungeni jijini Dodoma wakati akitambulisha wageni ambapo amemwambia “tunakushukuru sana kwa jinsi unavyoitangaza Tanzania, unafanya kazi nzuri, unazi-support pia timu zetu zinaposafiri huko na huko.”
Bongo Zozo amefika bungeni kama mgeni wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa.


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *Current track

Title

Artist