FOUNTAIN GATE WAMKABIDHI KOMBE PINDI CHANA
Written by Living Tarimo on April 11, 2023
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana akipokea Kombe la mabingwa wa Afrika kwa Shule za Sekondari kutoka kwa Nahodha wa Timu ya Fountain Gate Beatrice Charles ambao ndio wawakilishi wa Tanzania katika mashindano hayo yaliyomalizika hivi karibuni nchini Afrika Kusini. Mabingwa hao wa Afrika kwa Shule za Sekondari walioiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Kimataifa ya mpira wa miguu ya CAF nchini Afrika Kusini, wamealikwa bungeni na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Hayo yameelezwa leo na Waziri Balozi Pindi Chana kwenye hafla ya kuwapongeza na kuahidi kuwa wizara itatoa zawadi ya Tsh. milioni 10 kwao. Cc: @dmkglobal @makirijulius #Megafm2023TukoVizuri#weglobal🌎🇹🇿🇺🇸