GOMEZ WA SIMBA ATUMA CV JANGWANI
Written by Living Tarimo on June 20, 2023

Inadaiwa aliyekuwa Kocha wa Simba SC, Didier Gomes Da Rosa amekuwa miongoni mwa makocha waliyotuma CV kwenye Klabu ya Yanga akiomba kukabidhiwa mikoba ya Nabi.
Gomes aliachana na Simba SC Oktoba 26, 2021 siku chache tu baada ya Mnyama kuondoshwa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kichapo cha magoli 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana Benjamin Mkapa.