HATUJAVUNA KITU ILA TUAGANE

Written by on June 9, 2023

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally @ahmedally_ amewaomba Mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi leo kwenye mechi ya kufungia msimu 2022/23 dhidi ya Coastal ili watumie fursa hiyo kuwaaga Wachezaji na Wachezaji wawashukuru Mashabiki licha ya kukiri kwamba hakuna walichovuna kwakuwa Simba hana Kombe lolote msimu huu.
“Baada ya safari ndefu hatimaye leo tunafikia ukingoni, tulitamani safari yetu tuimalize kwa furaha lakini haijawa hivyo lakini hiyo haitupi sababu ya kuacha kuipa support Timu yetu pendwa”
“Wana Simba tukutane Uwanja wa Uhuru leo saa 9:30 tuwaage Wachezaji wetu na Wachezaji watuage sisi, japo hakuna tulichovuna tuwapongeze kwa kazi kubwa waliyoifanya na wao watushukuru kwa kuwashangilia katika nyakati zote “
“Pia sisi kama Familia ya Mashabiki tupate nafasi ya kuagana na kutakiana heri ya mapumziko, Love🦁Love🦁Love🦁”


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *Current track

Title

Artist