Cardi B Apishana na Bilioni 69

Written by on May 26, 2016

Cardi B ameliacha dili nono lenye thamani ya ($30M) zaidi ya TSh. Bilioni 69 kwa kujiengua kwenye nafasi ya uhusika mkuu wa filamu ya ucheshi ‘Assisted Living’ ambayo inatayarishwa chini ya kampuni ya Paramount Movies. Cardi anatajwa kuwa amefanya maamuzi hayo kutokana na kuzidiwa na ratiba zake.

Kwa mujibu wa tovuti ya Deadline, Cardi B amejiondoa kwenye nafasi hiyo ikiwa ni wiki mbili tu kuelekea siku ya kuanza uzalishaji (production) wa filamu hiyo. Kuondoka kwake kumeleta athari kubwa kwani kampuni ya Paramount Movies imebidi kuahirisha utengenezaji wa filamu hiyo. Hata hivyo wanasema hawajafungua mashtaka kwani wanaamini Cardi B anaweza kurejea tena siku za usoni.


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *Current track

Title

Artist