JKT YASITISHA KUPOKEA VIJANA
Written by Living Tarimo on June 14, 2023
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limesema vijana waliomaliza kidato cha sita na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo kwa mujibu wa sheria kwa mwaka huu na kushindwa kuripoti kwa muda uliopangwa, hawatapokelewa.
Kauli hiyo imetolewa mkoani Dar es Salaam na Brigedia Jenerali Hassan Mabena ambaye ni Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, wakati wa mkutano.wake na waandishi wa habari.
Brigedia Jenerali Mabena amesema vijana wote waliochaguliwa walitakiwa kufika katika kambi walizopangiwa kuanzia Juni Mosi, 2023 hadi Juni 11, 2023 lakini baadhi yao walishindwa kuripoti ndani ya.muda huo na badala yake wanaenda kuripoti hivi sasa.
Amesema jambo hilo linachelewesha kuanza kwa mafunzo, ndio maana JKT imesitisha kuwapokea vijana hao ili kuruhusu waliopo kwenye
kambi mbalimbali kuendelea na mafunzo.