JULIUS MALEMA HATUTAKI UNAFIKI WA ICC

Written by on March 24, 2023

Kiongozi wa Chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) na Mbunge wa Bunge la Afrika Kusini Julius Malema, amesema Rais wa Urusi Vladimir Putin anakaribishwa Afrika Kusini bila hofu huku akiahidi kumlinda licha ya hati ya kukamatwa iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) dhidi yake ikidai kuwa anahusika na uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na kuwahamisha Watoto kutoka Ukraine na kuwapeleka Urusi kinyume cha sheria.
Licha ya hati hiyo ya kukamatwa kwake iliyotolewa March 17,2023 ambapo Nchi 123 Wanachama wa Mahakama ya ICC ikiwemo Afrika Kusini wanatakiwa kumkamata Rais huyo wa Urusi na kumfikisha Mjini The Hague lakini Putin anatarajiwa kwenda Afrika Kusini kwenye Mkutano wa Kilele wa Nchi zinazounda BRICS (Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini) Mwezi August mwaka huu.
Malema amesema “Putin anakaribishwa hapa, na hakuna atakayemkamata Putin, ikibidi tutaenda kumpokea Airport hadi kwenye mkutano atatoa hotuba yake na kumaliza mkutano na tutampeleka Airport”
“Hatuwezi kuambiwa kitu na hawa Wanafiki ICC ambao wanawajua Wavunjifu halisi wa haki za Binadamu, wanawajua Wauaji wa Dunia hii, Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Tony Blair alikiri kuwa walifanya kosa kuhusu ishu ya Saddam Hussein, hawajahukumiwa hadi leo, George Bush bado yupo hawajahukumiwa”
“Obama amemuua Gaddafi na hakuna kilichotokea tupo hapa sasa huku Libya ikiwa imeharibiwa haiwezi kurudi kwenye ubora wake tena kisa Marekani tunajua vizuri NATO wakihusika sehemu hao ni Magaidi, tunajua Marekani ikisema ‘Tunaenda kuleta amani sehemu’, hiyo sehemu haiwezi kuwa na amani pale Marekani inapoenda eneo hilo”
“Hatuhitaji unafiki wa ICC hapa Afrika Kusini , Putin anakaribishwa, tunawajua Rafiki zetu, tunajua Watu waliotukomboa, waliotusaidia, silaha ambazo zilikuwa zinatumika wakati wa ukombozi wa Afrika Kusini zilitoka Urusi, Cuba walitusaidia Wanajeshi”


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *



Continue reading

Current track

Title

Artist