KAMATI YA BAJETI YATOA KAULI MUSWADA SHERIA YA KODI
Written by Living Tarimo on June 19, 2023

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Daniel Sillo amesema muswada wa sheria ya Fedha ni muswada unaowasilishwa bungeni kila mwaka. Hata hivyo, uzoefu wa Kamati yake unaonyesha kwamba muswada huo katika kipindi cha miaka 7 haujawahi kusomwa kwa mara ya kwanza na ya pili na kupitishwa ndani ya siku 14 kabla haujapitishwa na Bunge.
Sillo amesema hatua hii imekuwa inaleta changamoto ya muda kwa Kamati ya Bajeti kuuchambua, kufanya utafiti na kushirikisha wadau kabla ya kuwasilisha taarifa ya maoni yake bungeni.
Amesema mataifa ya jirani kama Kenya muswada huo huchukua si chini ya mwezi mmoja. Mfano muswada wa fedha wa mwaka 2023 wa Kenya ulichapishwa kwenye Gazeti la Serikali la Kenya Aprili 28, 2023 na hivi sasa ndio unajadiliwa na Serikali.
Cc: @dmkglobal @makirijulius
#Megafm2023TukoVizuri#weglobal🌎🇹🇿🇺🇸