KIWANGO CHA UKUAJI WA PATO LA TAIFA MWAKA 2022 KILIFIKIA 4.7%

Written by on June 15, 2023

MWIGULU: KIWANGO CHA UKUAJI WA PATO LA TAIFA MWAKA 2022 KILIFIKIA 4.7%

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Mwaka 2022 thamani halisi ya Pato la Taifa kwa bei za Mwaka 2015 lilifikia Tsh. Trilioni 141.9 ikilinganishwa na Tsh. Trilioni 135.5 Mwaka 2021

Kiwango halisi cha ukuaji wa pato la Taifa kilifikia 4.7% Mwaka 2022 ikilinganishwa na 4.9% Mwaka 2021. Sekta zilizokuwa na viwango vikubwa vya ukuaji kwa Mwaka 2022 ni Sanaa na Burudani (19.0%), Madini (10.9%), Fedha na Bima (9.2%), Malazi na Huduma ya Chakula (9%), na Umeme (7.6%)

Aidha, thamani ya Pato ghafi la Taifa linatarajiwa kufikia dola za Marekani Bilioni 85.42 Mwaka 2023/24


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *Continue reading

Current track

Title

Artist