LAZIMA TUWEKEZE KWENYE RASILIMALI ZETU
Written by Living Tarimo on July 7, 2023

Nchi ili iweze kuendelea ipo haja kuwekeza kwenye rasilimali watu
RAIS Mstaafu Jakaya Kikwete, amesema nchi ili iweze kuendelea ipo haja ya kuwekeza kwenye rasilimali watu, kwa kuwaendeleza katika elimu kuanzia ngazi ya awali hadi chuo kikuu, bila kusahau mafunzo ya ufundi.
Amesema nchi yeyote duniani iliyoendeleza kwa watu wake, kwa kuwaendeleza kielimu kwa ngazi ya chini hadi ya juu, ambao huja kutoa mchango katika uzalishaji sekta mbalimbali, hivyo vyuo vikuu ikiwamo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kina wajibu huo.
Kikwete ameyasema hayo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) maarufu SabaSaba, akisema maonesho hayo ni miongoni mwa fursa za kipekee kwa Watanzania, kutangaza bidhaa zinazozalishwa nchini pamoja na kuwaonesha wawekezaji kutoka nje, penye kuwekeza.
“Vyuo vikuu kazi yake kufundisha na moja ya kazi kubwa ni nchi kuendeleza rasilimali watu kupitia elimu ya msingi sekondari hadi vyuoni na vya mafunzo Ufundi. Hapo itapatikana rasilimali watu yenye ujuzi na mambo mengine huko yataenda kama kilimo, elimu tutafanya vizuri.
“Nikiwa Wizara ya .ambao ya Nje, nilikuwa na kauli mbinu ‘Tunafanya vizuri kuliko Jana’ hii ilikuwa kauli mbiu wakati huo. Yaani tuwekeze zaidi. Nimepita banda la UDSM nimeona ufumbuzi kwa kutumia rasilimaili zinazozaloshwa nchini, kwa kutengeneza bidhaa,” amesema Kikwete ambaye pia ni Mkuu wa chuo hicho.
Aidha, alikiasa chuo hicho kuendelea kufanya vizuri kwenye ufumbuzi kwa kuja na suluhisho, akisema nchi kubwa duniani wameendelea na kubuni vitu vikubwa ambavyo vimeanza kuvumbuliwa vyuoni na kufanya uchumi kujua.
Alipotembelea mabanda mbalimbali kama likiwamo la Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) pamoja na la UDSM, akisema biashara ni kuonesha kile kinachozalishwa na nchi husika, ili kijipatia soko.
“Upo umuhimu wa kukitangaza unachokizalisha hivyo
Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ni fursa kwa Watanzania, ili kutangaza kilichopo nchini hasa sekta ya biashara kwa kile tunachokitengeza nchini.