MAHAKAMA YAAMURU MWANAFUNZI ALIYEFUKUZWA TUDARCO KURUDISHWA CHUONI
Written by Living Tarimo on June 16, 2023

MAHAKAMA YAAMURU MWANAFUNZI ALIYEFUKUZWA TUDARCO KURUDISHWA CHUONI
–
Mahakama Kuu imeamuru Mwajuma Malulu, Mwanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Sheria-Chuo Kikuu Tumaini Dar es Salaam (TUDARCO) kurejeshwa chuoni na kuruhusiwa kufanya Mitihani ya Muhula wa 2 baada ya kufanyiwa Mtihani na mwenzie
–
Julai 21, 2022, Malulu (Mwanafunzi aliyekuwa Mwaka wa Mwisho) aliandikiwa barua na chuo, akitakiwa kujieleza, ambapo alikanusha kumruhusu Bahati Mfaume kumfanyia mtihani wowote. Mfaume alidai kuwa alimfanyia Malulu mtihani huo kwa kumuonea huruma kwa kuwa alikuwa nje ya Chuo, akimhudumia Mtoto wake mchanga
–
Seneti ya Chuo ilihitimisha kuwa Malulu alikuwa hatiani hivyo kumfukuza Chuo ambapo baadaye Malulu alituma maombi ili Mahakama itoe amri kwa #TUDARCO kufuta uamuzi wake na kumrejesha chuoni