MESSI AWAKACHA SAUDIA NA BARCA

Written by on June 7, 2023

Sky Sports wameripoti kwamba Mkali wa soka Lionel Messi anatarajiwa kujiunga na Timu ya Inter Miami ya Marekani baada ya mkataba wake na PSG kumalizika June 30 mwaka huu.
Pia Mwandishi wa Habari za Michezo Fabrizio Romano ameandika kwamba ni uhakika sasa kwamba Messi kazichinjia baharini Timu mbili zilizokua zikimtaka ambazo ni Al Hilal ya Saudi Arabia na Timu yake ya zamani ya Barcelona ambako Baba yake alionekana huko wiki hii kufanya mazungumzo lakini hayakufanikiwa na sasa Mwamba anaenda zake kwa Biden.
Mshindi huyu wa Ballon d’Or mara saba ambaye June 24 mwaka huu atatimiza umri wa miaka 36, ameifungia PSG magoli 32 ndani ya mechi zote 75 alizoshiriki. #MillardAyoSPORTS
Cc: @dmkglobal @makirijulius
#Megafm2023TukoVizuri#weglobal🌎🇹🇿🇺🇸


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *



Current track

Title

Artist