RAIS SAMIA ATEUA NA KUHAMISHA

Written by on June 9, 2023

Rais Samia Suluhu amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali ambapo amemteua Tito Mganwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Mussa Kilakala ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa wilaya ya Kaliua mkoani Tabora.
Rais Samia pia amefanya mabadiliko madogo ya vituo vya kazi ambapo amemhamisha Athumani Msabila kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga.
Mwantum Mgonja amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Mwamvua Mnyongo yeye amehamishwa kutoka wilaya ya Kaliua mkoani Tabora kwenda kuwa Katibu Tawala wa wilaya ya Chemba mkoa wa Dodoma.


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *



Current track

Title

Artist