SERIKALI YAAGIZA WALINDA AMANI WA UMOJA WA MATAIFA KUONDOKA KWA HARAKA
Written by Living Tarimo on June 17, 2023

Akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC), Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini #Mali, Abdoulaye Diop amevishutumu Vikosi vya kulinda Amani chini ya #UN (MINUSMA) kuwa chanzo cha matatizo na kuchochea migogoro ya ndani
Licha ya kuwa na Walinda amani takriban 13,000, #MINUSMA ambayo inamaliza muda wake Juni 29, 2023 imelaumiwa kwa kushindwa kuzuia machafuko na mauaji yanayofanywa na vikosi vya uasi vya Kijahidina, hivyo Mali imekataa kuongeza Mkataba mwingine
Nchi hiyo imeingia makubaliano na Vikosi vya Jeshi Binafsi la #WagnerGroup kutoka #Russia kwaajili ya kusaidia shughuli zake za Ulinzi na mafunzo ya Kijeshi, kitendo kinachotajwa kusababisha uhusiano mbaya kati yake na #Marekani
Cc: @dmkglobal @makirijulius
#Megafm2023TukoVizuri#weglobal🌎🇹🇿🇺🇸