TRUMP KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MARA YA PILI
Written by Living Tarimo on June 9, 2023

MAREKANI: TRUMP KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MARA YA PILI
–
Rais wa zamani wa Marekani, #DonaldTrump anatarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya #Miami akikabiliwa na makosa saba yakiwemo ya kumiliki nyaraka za siri za Serikali
–
Wakili wa Trump ameweka wazi kuwa Mwanasiasa huyo atafikishwa Mahakamani hapo Jumanne ya Juni 13, 2023 lakini bado wanasubiri Hati ya Mashtaka
–
Wakati huohuo, Idara ya Usalama inatarajia kukutana na wafanyakazi wa Trump ikiwemo walinzi wake, leo Juni 9, 2023 kwa ajili ya kupanga utaratibu wa msafara kuelekea Mahakamani