UCHAGUZI MDOGO KUFANYIKA KATA 14

Written by on June 14, 2023

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 14 za Tanzania Bara utakaofanyika Julai 13, 2023.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Ramadhani Kailima amesema, uchaguzi huo unafanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.
Kailima amezitaja kata hizo kuwa ni Ngoywa(Tabora), Sindeni, Potwe, Kwashemshi na Bosha (Tanga),
Mahege ( Pwani), Bunamhala (Simiyu), Njoro na Kalemawe( Kilimanjaro), Mnavira (Mtwara), Kinyika (Njombe),
Magubike (Morogoro) na kata ya Mbede (Katavi).
Amesema ratiba ya uchaguzi huo itaanza na utoaji wa fomu za uchaguzi kwa wagombea kuanzia Juni 24, 2023 hadi Juni 30 huku uteuzi wa wagombea watakaowania nafasi hizo ukifanyika Juni 30, 2023 na vyama vitakavyopata uteuzi vitaanza kampeni za uchaguzi Julai Mosi 2023 hadi Julai 12 , 2023.


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *Current track

Title

Artist