WATANZANIA WANAOISHI UJERUMANI WATAKIWA KUWA WAZALENDO

Written by on June 19, 2023

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amewataka Watanzania wanaoishi Ujerumani kuwa Wazalendo kwa kuitangaza vema nchi yao.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Ujerumani katika ukumbi wa Berlin Mariott.
Amewataka kuisemea vema nchi na kuwa Mabalozi kwa kuzitangaza fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na biashara na uwekezaji.
Dkt. Mwinyi amesema Serikali inaridhika na mchango wa wana Diaspora kwa maendeleo ya uchumi wa Taifa.
Amesema Serikali imeweka mfumo wa usajili kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi kwa usajili wa kidijitali kwa utambuzi, pia ipo tayari l kupokea ujuzi na fani mbalimbali za Watanzania waliojifunza katika nchi mbalimbali kwa kujenga uchumi wa nchi.
Rais Mwinyi anafanya ziara nchini Ujerumani ambapo akiwa nchini humo tayari amehudhuria ufunguzi wa mashindano ya Dunia ya Olimpiki Maalumu akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Cc: @dmkglobal @makirijulius
#Megafm2023TukoVizuri#weglobal🌎🇹🇿🇺🇸


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *Current track

Title

Artist